You are currently viewing MEJJA ATOA ANGALIZO KWA MASHABIKI ZAKE KUWA MAKINI NA MATAPELI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

MEJJA ATOA ANGALIZO KWA MASHABIKI ZAKE KUWA MAKINI NA MATAPELI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Msanii nyota nchini Mejja kwa nyingine amewatolea uvivu baadhi ya watu wanaotumia jina lake vibaya kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.

Kupitia  ukurasa wake instagram Mejja amesema akaunti zote ambazo zinatumia jina lake kwenye mtandao wa facebook na twitter ni batili huku akiwataka mashabiki zake wawe waangalifu na matapeli wanaotumia chapa yake kujitakia makuu.

Kauli ya Mejja imekuja mara baada ya ukurusa mmoja kwenye mtandao wa twitter unaotumia jina lake kumwagia sifa diamond platinumz jambo ambalo lilipelekea ukurasa rasmi wa lebo ya wcb inayomilikiwa diamond kuchapisha ujumbe huo kwenye mitandao ya kijamii.

Hii sio mara ya kwanza kwa mejja kuwaonya watu dhidi ya akaunti feki zinazotumia jina lake kwenye mtandao wa facebook na twitter kwani mwaka wa 2020 alifanya hivyo tena mara  baada ya jamaa mmoja kumtuhumu kuwa alidinda kutokea kwenye interview yake licha ya kumlipa shillingi elfu 12.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke