You are currently viewing Mejja awaonya mashabiki dhidi ya matapeli mtandaoni

Mejja awaonya mashabiki dhidi ya matapeli mtandaoni

Staa wa muziki nchini Mejja ametoa angalizo kwa mashabiki zake kuwa makini na baadhi ya matapeli wa mitandao wanaotumia jina lake kujitakia makuu.

Kupitia instastory yake,Hitmaker huyo wa “Usiniharibie Mood” amewaonya mashabiki kwamba hausiki kwa chochote na wala hatowajibika kwa watu wasio waaminifu wanaojifanya kuwa yeye.

Aidha amesema hajawahi kuwa na akaunti yeyote kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na Tiktok huku akisisitiza kuwa mtandao pekee ambao ana umiliki wa akaunti ni Instagram.

Mejja ametoa kauli hiyo mara baada ya mtumiaji mmoja wa Facebook anayetumia jina lake kuchapisha taarifa ya kumpongeza msanii Trio Mio ambaye kwa mujibu wa akaunti hiyo alipata alama ya D- kwenye mtihani wa KCSE.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke