Nyota wa muziki nchini Mejja ametangaza ujio wa album yake mpya ambayo ana mpango wa kuiachia hivi karibuni.
Akiwa kwenye moja ya Interview mkali huyo wa “Siskii” amewataarifu mashabiki zake wawe tayari kwa Album hiyo ambayo ameanza kuifanyia kazi.
Mejja amedai kuwa amechukua hatua ya kuiachia album hiyo kutokana na uhitaji wa mashabiki zake huku akisema itakuwa moto wa kuotea mbali.
Hivyo mashabiki wa nyota huyo mkae mkao wa kula kuipokea album yake hiyo mpya ambayo amedai itaingia sokoni mwakani.