You are currently viewing MEMBER WA SAILORS GANG SHALKIDO ATANGAZA KUACHA MUZIKI

MEMBER WA SAILORS GANG SHALKIDO ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Member wa kundi la Sailors gang, Shalkido ametangaza kuachana kabisa na masuala ya muziki.

Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa instagram,Shalikido amesema amechukua uamuzi huo baada ya kugundua kuwa muziki wake umepoteza mvuto kwenye jamii, hivyo ni wakati wake wa kupumzika na kuacha wasanii wengine waendelee.

“Baada ya muda mrefu kutafakari kuhusu kazi yangu ya muziki, nimegundua kuwa muziki wangu hauna mashiko.”

“Kwa hivyo nimeamua kubadilisha kazi yangu kwa kufanya kitu kitakachoniridhisha zaidi maishani. Kwa mashabiki wangu wote walioniamini, samahani sana kuwaangusha.”, Ameandika kupitia instastory yake.

Taarifa Shalkido kustaafu muziki imewaacha mashabiki zake na mshangao kwani wengi wamekuwa na kiu ya kutaka kusilikiza nyimbo za kundi la Sailors gang.

Baadhi ya mashabiki wa shalkido wanahisi huenda msanii huyo anatengeneza mazingira ya kuzungumziwa nchini ili aweze kuachia singo yake mpya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke