You are currently viewing MENEJA VAGA AMKINGIA KIFUA STIVO SIMPLE BOY KWA TUHUMA ZA WIZI

MENEJA VAGA AMKINGIA KIFUA STIVO SIMPLE BOY KWA TUHUMA ZA WIZI

Meneja wa Stivo Simple Boy Vaga amevunja kimya chake kuhusu tuhuma zilizotembea mtandaoni kuwa msanii wake alimuiba mpenzi wa mtu.

Katika mahojiano yake na Captain Nyota vaga amesema madai ya Stivo kumchukua mpenzi wa mtu hayana ukweli wowote bali yanatumiwa na baadhi ya watu mtandaoni  kama daraja la kupata umaarufu kwenye vyombo vya habari nchini.

Aidha amesema Stivo alimpata mpenzi wake kwa njia ya halali huku akisema msaniii huyo yupo mbioni kufunga ndoa na mchumba wake ikiwa ni siku chache zimepita tangu wavishane pete ya uchumba.

Kauli ya Vaga imekuja mara baada ya wanaume wawili kujitokeza kwenye nyakati tofauti na kudai kuwa stivo aliwaibia mpenzi wao kitu ambacho ambacho stivo mwenyewe alikanusha vikali mapema wiki hii.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke