Meneja wa msanii Happy C, Mwaringa amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ugomvi wake na msanii huyo kutoka 001 Music.
Katika mahojiano yake na podcast ya Captain Nyota, Mwaringa ambaye yupo chini ya Uptown Records amekiri kuwa Happy C alikuwa na deni lake kitu ambacho amedai kuwa lilimfanya kutokuwa na maelewano mazuri naye ila kwa sasa wamezika tofauti zao baada ya Happy C kumlipa pesa zake.
Mbali na hayo Mwaringa amedokeza ujio wa EP mpya kutoka kwa Happy C ndani ya mwaka huu EP ambayo kwa mujibu wake imekamilika kwa asilimia mia ila kwa sasa ni jambo la kuiachia tu.
Hata hivyo amesema baada ya EP ya Happy C kutoka, kuna album ambayo pia itafuata ambayo kwa sasa inatayarishwa na chini ya prodyuza Totti.
Utakumbuka juzi kati Mwaringa alitumia mtandao wake wa facebook kudai kwamba hajalipwa pesa zake na lebo ya 001 Music jambo lilompelekea kufuta video zote za nyimbo za msanii wake Happy C youtube.