Meneja wa Harmonize, Mchopa amemkingia kifua Staa wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz kufuatia watu kumkosoa mitandaoni kwa kupiga picha na bendera ya kibaguzi.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Mchopa amefunguka kuwa ni wazi Diamond hakukusudia kufanya hivyo huku akiwasihi watu kutolipa nguvu suala hilo na badala yake wajaribu kukosoa kwa njia nzuri ya kujenga.
Utakumbuka mapema wiki iliyopita Diamond Platnumz aligonga vichwa vya habari mara baada ya kukosolewa mitandaoni kwa kutumia bendera yenye utata katika video ya wimbo wake mpya wa Gidi.
Bendera hiyo ni ya kundi la Shirikisho la majimbo ya kusini mwa Marekani ambalo lilipigania kudumisha utumwa wa watu weusi kati ya mwaka wa 1960 & 1961 na inaonekana ina tafsiri ya moja kwa moja kwamba Diamond aliungana na wazungu katika kuwapiga vita ndugu zake Weusi.