You are currently viewing MENEJA WA KUNDI LA MBOGI GENJE AMVUA NGUO KRG THE DON KISA KUWAADA WAKENYA

MENEJA WA KUNDI LA MBOGI GENJE AMVUA NGUO KRG THE DON KISA KUWAADA WAKENYA

Meneja wa kundi la Mbogi Genje Eastlando President amemtolea uvivu msanii KRG The Don kwa madai ya kuwadanganya wakenya kuwa yeye ndiye mmliki wa ukumbi wa burudani wa Casavara.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Eastlando president amesema kuwa mmiliki halisi waCasavara ni msanii wa dancehall kutoka jamaica Konshens ila KRG amepewa kazi ya kuipromote ukumbi huo wa starehe.

Eastlando President ameenda mbali kumtaka KRG aache suala la kujigamba na badala ajifunze kuwa heshimu watu wengine kwani pesa ambazo analipwa na konshens zimempa kiburi.

Kauli ya Eastlando president imekuja mara baada ya KRG The Don kushindwa kuwalipa wasanii wa kundi la Mbogi Genje pesa zao baada ya kuwashirikisha kwenye wimbo wake uitwao Zible ambao ulikuwa umefutwa kwenye mtandao kwa madai ya hakimiliki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke