You are currently viewing Meneja wa muziki nchini Uganda James Mulwana afunguka kuvunja mkataba na msanii Ronald Alimpa

Meneja wa muziki nchini Uganda James Mulwana afunguka kuvunja mkataba na msanii Ronald Alimpa

Misala haiishi kwa msanii Ronald Alimpa kutoka nchini Uganda, 2022 unakuwa mwaka mbaya kwake. Baada ya msala wa ajali ya barabarani uliompelekea kulazwa hospitalini, sasa ni zamu ya meneja wake James Mulwana.

Mulwana ambaye amekuwa akimsimamia kimuziki ametangaza kuvunja mkataba na msanii huyo kutokana na tabia yake ya utukutu.

Katika mahojiano yake hivi karibuni meneja huyo wa muziki amesema anasubiri Alimpa apate nafuu kutokana na majeraha mabaya aliyopata kwenye ajali ya barabarani mwezi mmoja uliopita kisha atasitisha utoaji wa huduma kwa msanii huyo.

“We had parted ways but I came back when he got into an accident. With his current attitude, I can’t continue with him. I will finalize our business this month,” Alisema Mulwana

Kauli ya James Mulwana imekuja mara baada ya Hitmaker huyo wa “Seen don” kumporomoshea matusi ya nguoni mama yake mzazi kwa hatua ya kutumia vibaya pesa alizochangiwa na wahisani kugharamia matibabu yake hospitalini.

Aidha, baada ya Alimpa kumvunjia heshima mama yake mzazi, mganga wa kienyeji nchini Uganda Mama Fina ambaye amekuwa akimsaidia msanii huyo kifedha aliamua pia kusitisha kutoa huduma kwake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke