You are currently viewing MENEJA WA OTILE BROWN AFUNGUKA JUU YA KUFUTWA KWA NYIMBO ZA STAA HUYO YOUTUBE

MENEJA WA OTILE BROWN AFUNGUKA JUU YA KUFUTWA KWA NYIMBO ZA STAA HUYO YOUTUBE

Meneja wa otile brown Noriega amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kufutwa kwa nyimbo za msanii huyo kwenye mtandao wa youtube.

Akiwa kwenye moja ya interview meneja huyo amesema kama uongozi wa otile brown wameshangazwa na hatua ya nyimbo za staa huyo kufutwa kwenye mtandao wa youtube na aliyezi-upload ambapo ameahidi kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu ili kuhakikisha waliohusika wanakabiliwa kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo Noriega amepuzilia mbali madai yanayotembea mitandaoni kuwa otile brown anatumia suala la nyimbo zake kufutwa kwenye mtandao wa youtube kuupromote kazi yake mpya kwa kusema kwamba suala hilo sio kiki kama inavyodaiwa kwani otile brown huwa hatumii kiki kutangaza muziki wake.

Nyimbo ambazo zilifutwa kwenye channel ya youtube ya msanii huyo ni pamoja na Dusuma, Such Kinda of love, Chaguo la moyo wangu, Aiyana na nyingine nyingi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke