Meneja wa msanii Recho Ray, Saka ametangaza kuacha kufanya kazi na msanii huyo kwa kile kinachodaiwa kuwa hasara ambayo amepata tangu aanze kusimamia kazi zake za muziki.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya Saka kuwekeza pesa nyingi kwa Recho Rey lakini hajaweza kurudisha hata senti moja kwani msanii huyo hajaweza kutumbuiza kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na katazo la kuzuia msambao wa corona.
Sasa akiwa kwenye moja ya interview Recho Rey amesema anatafuta meneja ambaye yuko vizuri kifedha ili aweze kusimamia kazi zake za muziki.
“Niko uhuru kufanya kazi na mtu yeyote ambaye ana pesa kuwekeza kwenye muziki wangu. Cha muhimu sasa hivi ni mtu ambaye yupo tayari kutengeneza pesa kupitia brand yangu ya muziki:….alisema Recho Rey kwenye moja ya interview.
Ikumbukwe kipindi cha nyuma Recho Rey alikuwa anafanya kazi na meneja wa sasa wa msanii Crysto Panda aitwaye Apple lakini walikuja wakaachana baada mrembo huyo kuingia ubia wa kufanya kazi na meneja mwingine aitwaye Saka.