You are currently viewing MFUMO WA TWO-FACTOR AUTHENTICATION KUWA LAZIMA KATIKA AKAUNTI ZOTE ZA GOOGLE

MFUMO WA TWO-FACTOR AUTHENTICATION KUWA LAZIMA KATIKA AKAUNTI ZOTE ZA GOOGLE

Mwezi wa tano mwaka huu Google ilitoa tamko watumiaji wote wanaotumia huduma za Google kuweka mfumo wa Two-Factor authentication (two-step verification) ili kuboresha usalama wa akaunti na ilisema mwisho wa mwaka huu itaweka iwe ni lazima kwa watumiaji wake wote.

Mfumo wa 2FA unasaidia kuweka ulinzi wa ziada, endapo hacker au mtu akipata Password yako, atashindwa kuingia kwa sababu atalazimika kuandika namba maalum ambayo inatumwa katika simu yako kwa njia ya SMS, au App ya Google Search na Google Authenticator.

Google imekumbusha akaunti zote ambazo hazijaweka mfumo wa 2 Factor Authentication zitalazimika kuwekwa mfumo huo kwa lazima. Endapo kama uliweka namba ya simu ya zamani utashindwa kuingia kwenye akaunti yako mpaka ukiweka PIN ambayo itatumwa kwenye namba hiyo.

Zaidi ya Akaunti Milioni 150 zikiwemo akaunti za Content Creators Milioni 2 wa YouTube ambao hawajaweka mfumo huo; zitafungiwa na zitalazimika kutumia mfumo mpya kwa lazima.

Kuepuka kukosa akaunti ni vyema kuithibitisha namba ambayo imesajiliwa katika 2 Factor na devices zote ambazo umeziunganisha na akaunti yako kabla ya kufungwa rasmi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke