You are currently viewing MICHUANO YA AFCON KUENDELEA LEO NCHINI CAMEROON

MICHUANO YA AFCON KUENDELEA LEO NCHINI CAMEROON

Michuano ya fainali za mataifa ya Afrika AFCON zilianza kutimua vumbi jana katika miji ya Cameroon kwa michezo miwili kuchezwa.

Mchezo wa mapema katika dimba la Olembe wenyeji indomitable lions Cameroon walianza vema kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Burkina Faso waliotangulia kupata bao.

Mchezo wa pili katika kundi hilo umewakutanisha Ethiopia dhidi ya cCape Verde na Ethiopia kukubali kichapo cha bao, 1 -0 likiwekwa kimiani na Juao Tavares

Michuano hiyo itaendelea tena leo kwa michezo mitatu Senegal dhidi ya Zimbabwe, Guinea dhidi ya Malawi na mchezo wa mwisho ni Moroko dhidi ya Ghana.

Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni Algeria akichukua mbele ya Senegal mwaka 2019 nchini Misri kwa bao la Baghdad Bounedjah

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke