You are currently viewing MICROSOFT YAWEKA MFUMO WA KUTOA ONYO KUHUSU USALAMA WA CHROME.

MICROSOFT YAWEKA MFUMO WA KUTOA ONYO KUHUSU USALAMA WA CHROME.

Browser ya kuperuzi ya Google Chrome inatumika na zaidi ya watumiaji Bilioni 2 ambao wanaitumia sana. Hivi karibuni kuna kesi inaendelea baada ya tetesi kuonyesha zaidi ya watumiaji Bilioni 2 wa Google Chrome wapo katika hatari ya data zao kukusanywa sana mitandaoni kutokana na baadhi ya madhaifu ambayo yapo katika browser ya Chrome.

Microsoft imeweka mfumo wa kutoa onyo kuhusu Usalama na Uhakika wa Chrome, pale watumiaji wa Windows wakipakua app ya Chrome. Microsoft imeamua kuwa wazi na kupambana kuzuia watumiaji wa Windows kutumia Google Chrome.

Mwaka huu Chrome imepata hack nyingi kuliko kipindi chote na ni kwa sababu bado kuna madhaifu mengi Google imeacha katika Chrome ili kulinda mfumo wake wa matangazo na kukusanya data.

Ishu kubwa inayoendelea, Browser nyingi kama vile Mozilla, Safari, Brave na Opera zimeweka mfumo mpya wa kuzuia websites kusoma cookies za website nyingine, mfumo wa kuzuia trackers, Third-Party tracking, na mfumo wa AI ya kuweka usiri wa mtu anachoperuzi kwa mfumo wa encryption.

Google pekee yake ndio imeacha madhaifu hayo japo browser yake inaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi duniani na kila mwaka wanaongezeka, lakini bado hakuna maboresho ya kiusalama.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke