Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike sonko amejipata akitupiana maneno makali mtandaoni na Deejay maarufu nchini DJ Kalonje.
Hii ni baada ya DJ Kalonje kuibuka na kumtaja Jaguar na Sonko kama wanasiasa ambao walishindwa kumsaidia kurejesha studio yake iliyonyakuliwa na bwenyenye mmoja jijini Nairobi licha ya kuwasilisha lalama zake kwao.
Sasa Kupitia ukurasa wake Instagram Sonko ameamua kutoa ya moyoni kwa kupuzilia mbali madai hayo, akisema kwamba ameshangazwa na hatua ya Kalonje kumzushia madai ya uongo ikizingatiwa kuwa hajawahi kumuomba usaidizi wowote wakati anahudumu serikalini.
Sonko hata hivyo amemporomoshea mvua ya matusi Kalonje akimtaka akome kumchafulia jina mtandaoni huku akienda mbali zaidi na kuhoji kuwa huenda stress za mapenzi ndio zinamsumbua DJ huyo ambaye ameonekana kuwa na uwezo mdogo wa kufikiria.
“Usaidiwe na politician kwani we ni slay queen? Nakama umekuwa shoste utuambie!”
“Mimi sio red cross ati lazima nikusaidie.”
“Mafeelings zako na madepression zako za ma dame peleka mbali na mimi.” Aliandika Instastory yake.
Kauli ya Sonko inakuja mara ya DJ Kalonje kudai kuwa manyanyaso ambayo Sonko alimpitisha pamoja na marehemu baba yake mzazi ndio chanzo cha mwanasiasa huyo kukumbwa na skendo za kisiasa kiasi cha kushindwa hata kumaliza hatamu yake ya uongozi kama Gavana wa Kaunti ya Nairobi.