Msanii wa Sailors Gang, Miracle Baby ametuhumiwa kumtelekeza binti yake mwenye umri wa miaka miwili kwa kushindwa kumpa mahitaji ya msingi.
Tuhuma hizo zimeibuliwa na baby mama wake Tash Baby kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo amedai kwamba mpenzi mpya wa msanii huyo anayefahamika kama Carol amekuwa kizingiti kwa mtoto wake kupata mahitaji ya msingi kutoka kwa baba yake.
Tash Baby amesema kila mara anapojaribu kumpigia simu Miracle Baby Carol ndiye ushika simu na badala yake amekuwa akimtupia kila aina ya matusi aache kumfuta mume wake kwani hakuwa kipindi ambacho alikubaliana kuzaa na msanii huyo.
Hata hivyo Miracle Baby hajatoa tamko lolote kuhusiana na tuhuma hizo zilizoibuliwa na Baby Mama wake ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na Baby mama wake wengi wakihoji kwamba huenda ni kiki ya kumrudisha Miracle Baby kwenye kiwanda cha muziki nchini baada ya ukimya wa muda mrefu.