You are currently viewing MISS CASHY AANIKA MADHAIFU YA KHALIGRAPH JONES

MISS CASHY AANIKA MADHAIFU YA KHALIGRAPH JONES

Rapa wa kike nchini Miss Cashy amemchana baby daddy Khalighraph Jones kwa mara nyingine kwa madai ya kushindwa kumhudumia mtoto wake.

Kupitia mfululizo wa post zake instagram Cashy amekanusha tuhuma zilizoibuwa na walimwengu kwamba anataka kuvunja ndoa ya Papa jones kwa kueleza kuwa mtoto wake alizaliwa miezi kadhaa baada ya khaligraph jones kumpata binti wake wa kwanza.

Katika hatua nyingine hitmaker huyo wa ngoma ya “Mi Casa Sucasa” pia ameweka wazi mpango wa kuanza kuzitafuta kampuni ambazo rapa huyo ameingia ubia kufanya naye kazi  ili aweze kupata mgao ambao utamsaidia kutoa mahitaji ya msingi kwa mtoto wao.

Hii sio mara ya kwanza Cashy kumsuta vikali Khaligraph Jones kwa madai ya kumtelekeza mtoto wake mwaka wa 2021 alidai rapa huyo alikuwa akitoa visingizo ya kutotoa matunzo kwa mtoto wao kutokana na kanuni za kudhibiti msambao wa corona zilizowekwa na serikali.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke