Female Rapper kutoka Kenya Miss Cashy amedai kuwa licha ya vipimo vya DNA kubaini kuwa rapa Khaligraph Jones ndiye baba wa mtoto wake rap huyo amekataa kutoa matunzo kwa mtoto wake huyo.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni amesema mwaka wa 2021 alifanya vipimo vya DNA baada ya rapa huyo kumshinikiza afanye hivyo ambapo amedai kuwa amelazimika kuhama nairobi kwa ajili ya kumshughulikia mtoto wake huyo.
Mrembo huyo amesema hataki tena kuzungumzia suala la Papa Jones kukimbia majukumu ya kumlea mtoto wake kwani amechoka kuonekana anatafuta uhuruma kwa mashabiki wa rapa huyo.
Ikumbukwe Miss Cashy amekuwa akimshinikiza Khaligraph Jones ajukumikie mahitaji ya msingi ya mtoto wao ila rapa huyo amekuwa kimya juu ya swala hilo na hata kukwepa maswali ya waandishi wa habari anapokuwa kwenye mahojiano mbali mbali.