You are currently viewing MISS CASHY: KHALIGRAPH JONES AMETIA NIA YA KUANZA KUMPA MTOTO WAKE MATUNZO LICHA YA KUMKANA

MISS CASHY: KHALIGRAPH JONES AMETIA NIA YA KUANZA KUMPA MTOTO WAKE MATUNZO LICHA YA KUMKANA

Baby mama wa Rapa Khaligraph Jones, Miss Cashy amedai kwamba rapa huyo kwa sasa ameanza kuonyesha nia ya kutaka kumhudumia mtoto wake ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu amkane hadharani kwamba hamfahamu kabisa.

Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Miss Cashy amesema mwenyezi Mungu amejibu maombi yake kwa kumfanya rapa huyo abadili mawazo yake juu ya mtoto wake ambaye alikuwa amemtelekeza kwa muda mrefu.

Mrembo huyo ameenda mbali na kusema kwamba kwa sasa rapa huyo anajaribu kusafisha jina lake mbele ya mashabiki kwa kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari licha ya kutumia suala la kumtelekeza mtoto wake kujitafutia kiki.

Hata hivyo amesema anaamini kwamba Khaligraph Jones atakuja kumpa mtoto wao  mahitaji ya msingi hata ikichukua muda mrefu.

Kauli ya Miss Cashy imekuja mwezi mmoja baada kujitokeza na kudai kwamba mwaka wa 2021 Khaligraph Jones alimshinikiza wafanye vipimo vya dna kwa mtoto wao ambapo ilikuja akabaini kuwa rapa huyo ndiye Baba wa mtoto wake.

Ikumbukwe Miss Cashy amekuwa akimshinikiza Papa Jones  ajukumikie mahitaji ya msingi ya mtoto wao ila rapa huyo amekuwa kimya juu ya swala hilo na hata kukwepa maswali ya waandishi wa habari anapokuwa kwenye mahojiano mbali mbali.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke