Mama mtoto wa Khaligraph Jones, Cashy Karimi amefichua kuwa ana mpango kumshtaki rapa huyo baada ya kukataa kutoa matunzo kwa mtoto wao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Cashy amechapisha picha yake akiwa katika Mahakama ya Milimani na kuandika caption inayosomeka, “Ukiitwa unaitika uilvyo, ukiwa mbali njoo na champali. Ujasiri hutoka kwa Mungu, mwamuzi halisi na mlinzi wa haki. Mungu wa milimani na mabondeni, tangulia mbele yetu.”
Ujumbe huo umetafsiriwa na ulimwengu kuwa huenda mrembo huyo amemfungulia mashtaka khaligraph jones kwa hatua ya kukwepa kutoa mahitaji ya msingi kwa mtoto wake.
Wawili hao wana mtoto wa kiume pamoja,aitwaye Xolani lakini Cashy amekuwa akishikilia kuwa Khaligraph amekuwa akimtelekeza mtoto wake, huku akiwahudumu watoto wake wengine.
Baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii hata hivyo wamemhimiza Cashy kuendelea na hatua ya kumpigania motto hadi pale khalighraph jones atakaporidhia suala la kutoa matunzo kwa mtoto wao.
“Wewe peke yako ndiye unayejua unapitia nini, usiwasikilize watu hawatakuwekea chakula, mvulana anahitaji mambo mengi pigana naye”
“Pigana kwa ajili ya mtoto wako wakati wote … Yule yule anayekuambia usishtaki mwanamume au kumburuza mahakamani hatamlisha mwanao”
“Usijaribu kupata watoto wakati huwezi kuwatunza …