You are currently viewing MJENGO WA KIFAHARI WA MSANII RINGTONE KUPIGWA MNADA KWA TAKRIBAN SHILLINGI MILLIONI 80

MJENGO WA KIFAHARI WA MSANII RINGTONE KUPIGWA MNADA KWA TAKRIBAN SHILLINGI MILLIONI 80

Mjengo wa kifahari wa msanii wa nyimbo za injili nchini Ringtone ulioko mitaa ya Runda jijini Nairobi imepiga mnada kwa shillingi millioni 80 na kampuni moja ya wanasheria.
 
Hatua hii inakuja siku chache baada ya Ringtone kupewa notisi ya siku 10 ya kuondoka kwenye mjengo huo wenyewe utata la sivyo ahamishwe kwa nguvu.
 
Kulingana na barua iliyotolewa na kampuni ya mawakili ya AGN Kamau Advocates,  nyumba ambayo ringtone anaishi kwa sasa ni ya raia wa Sweden kwa jina Mona Ingegard aliyefariki mwaka wa 2007 na Ringtone alinunua nyumba hiyo bila kufuata njia sahihi.
 
Hata hivyo Ringtone mpaka sasa hajatoa tamko lolote kuhusiana madai ya mjengo wake wa kifahari kupigwa mnada.
 
 
 
 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke