Mjukuu wa hayati Bob Marley aitwaye Joseph ‘Jo Mersa’ Marley amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 31.
Mwimbaji huyo wa muziki wa Reggae amekutwa akiwa amefariki kwenye gari lake Disemba 27.
Sababu ya kifo chake bado haijathibitishwa lakini kituo cha Redio WZPP cha mjini Florida kimeripoti kwamba kifo chake kimetokana na maradhi ya Pumu (Asthma) japo Polisi bado hawajatoa taarifa za uchunguzi.
Joseph Mersa Marley alitumia miaka yake ya awali huko Jamaica, ambapo alihudhuria Shule ya Maandalizi ya Watakatifu Peter na Paul.
Kisha akahamia Florida ambapo alikuwa mwanafunzi katika Shule ya Upili ya Palmetto. Akiwa Miami Dade College alisomea studio engineering.
Mwaka 2014 alitoa EP iitwayo Comfortable na 2021 akatoka na Eternal.