Mke wa mwanamuziki Ali Kiba, Amina Khalef amewasilisha kesi mahakamani ya kutaka kutengana na mume wake.
Amina anatajwa kuwasilisha kesi hiyo ya talaka katika mahakama ya kadhi mjini Mombasa mwezi uliopita baada ya kudumu kwa miaka mitatu kwenye ndoa huku shauri hilo la talaka likitaka Ali Kiba ampe Amina kiasi cha shillingi laki 2 za Kenya kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya watoto wao wawili.
Inaelezwa kuwa miongoni mwa sababu za kuvunja ndoa ya Amina na Ali Kiba ni kuwa na msongo wa mawazo pamoja na mwanamuziki huyo kutotekeleza majukumu yake kama mume.
Hata hivyo Ali Kiba amepewa siku 15 awe ametoa majibu katika mahakama ya kadhi mjini Mombasa.
Wawili hao walioana mwaka wa 2018, kwa sheria za Kiislamu ambapo waliandaa sherehe kubwa iliandaliwa mji Mombasa huku sherehe hiyo akitajwa kama harusi ghali zaidi Afrika Mashariki.