You are currently viewing Mke wa Miguel, Nazanin Mandi aomba talaka baada ya miaka 3 ya ndoa

Mke wa Miguel, Nazanin Mandi aomba talaka baada ya miaka 3 ya ndoa

Ndoa ya mwanamuziki Miguel na Nazanin Mandi imefikia mwisho, Mandi ameomba Talaka baada ya ndoa hiyo kudumu kwa miaka mitatu. Sababu Kuu iliyoandikwa kwenye ombi la mwanadada huyo ni (Irreconcilable Differences) yaani tofauti baina ya wana ndoa ambazo haziwezi kutatuliwa.

Kama utakumbuka mwaka 2021, Wawili hao walianika wazi utengano wao lakini Februari mwaka huu walimaliza tofauti zao. Pamoja wamedumu kwa miaka 17 na walivishana Pete ya uchumba mwaka 2016. Aidha ndoa yao ambayo ilifungwa 2018 ilikuwa na makubaliano ya mgawanyo wa mali (Prenuptial agreement) hivyo hilo litatokea.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke