You are currently viewing MKE WA MSANII BAHATI, DIANA B AZUA GUMZO MTANDAONI

MKE WA MSANII BAHATI, DIANA B AZUA GUMZO MTANDAONI

Siku chache baada ya mke wa msanii Bahati, Diana B kutangaza kujiunga na tasnia ya muziki nchini ambapo alienda mbali zaidi na kuachia wimbo wake wa kwanza uitwao Hatutaachana, mwanamama huyo amezua gumzo mitandaoni.

Hii ni baada ya  mume wake Bahati kwenye moja ya interview kutangaza bei ya diana marua kutumbuiza kwenye tamasha lolote ambalo ataalikwa.

Bahati alinukuliwa akisema kwamba kwa yeyote ambaye atamhitaji mke wake diana b kwenye shoo atalazimika kulimpia kiasi cha shillingi laki   8 kwa shoo moja.

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kupuzilia mbali bei hiyo ya shoo kwa kusema mrembo huyo hana cha kuwapa mashabiki wa muziki nchini ikizingatiwa kuwa hana kipaji cha muziki.

Hata hivyo Diana B amewatolea wanaopinga safari ya muziki kwa kusema kwamba wataendelea kugonja anguko lake kwenye muziki ikizingatiwa tayari waandaji wa matamasha wameanza kumpa michongo ya kutumbuiza kwenye shows zao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke