You are currently viewing MKE WA MWANAMUZIKI JUSTIN BIEBER AFUNGUKA UGONJWA UNAOMSUMBUA

MKE WA MWANAMUZIKI JUSTIN BIEBER AFUNGUKA UGONJWA UNAOMSUMBUA

Mke wa mwimbaji Justine Bieber, Hailey Bieber amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu changamoto yaki afya iliyomkabili mwezi uliopita, ambayo ilimfanya moja kwa moja afikiri kuwa amepata ugonjwa wa kiharusi.

Utata wa kukumbwa na ugonjwa wa Kiharusi kwa Hailey, uliishia hospitalini ambako madaktari walibaini kuwa alikuwa na tundu kwenye moyo wake.

Kwa mujibu wa ripoti za TMZ inaelezwa kuwa, Hailey alikimbizwa hospitali baada ya kupata dalili zinazofanana na kiharusi na hata baadae madaktari kubaini kuwepo kwa damu iliyoganda kwenye ubongo wake.

“TIA”, tatizo linalofahamika kama kiharusi kidogo (a mini-stroke) jambo lililorandana na mawazo yake ya awali punde baada ya kuanza kuumwa.

Baada ya uchunguzi wa kina wa madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu, hatimaye Hailey alibainika kuwa na kitu kiitwacho PFO kwa lugha ya kitabibu, yaani tundu/mwanya mdogo kwenye moyo wake.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 25 alifanyiwa upasuaji ambao ulikwenda vizuri na kumfanya walau kurejea kwenye hali yake kawaida.

Hailey anasema amekuwa akitumia dawa za kusaidia damu kutiririka vizuri kwenye mishipa (Blood thinners) kila siku tangu tukio hilo ili kuepuka changamoto hiyo kujirudia tena.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke