Mlinzi wa rapa Lil Wayne kutoka Marekani ameamua kutimba mahakamani na kufungua mashtaka dhidi ya Lil Wayne ambaye anadaiwa kumtishia silaha mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka wa 2021.
Kwa mujibu wa TMZ, moja ya walinzi wa rapa huyo aliwaambia polisi kwamba Lil Wayne aliingia kwenye majibizano na bodyguard wake akiwa nyumbani kwake mjini Hidden Hills, California.
Hii ni baada ya Lil Wayne kumtuhumu bodyguard huyo kupiga picha ya nyumba yake na kuzivujisha kwenye vyombo vya habari.