You are currently viewing MOJI SHORT BABA AKIRI KUUMIZWA NA KUNDI LA KELELE TAKATIFU KUVUNJIKA

MOJI SHORT BABA AKIRI KUUMIZWA NA KUNDI LA KELELE TAKATIFU KUVUNJIKA

Msanii wa nyimbo za injili nchini Moji Short Baba amefunguka masaibu aliyomkumbana nayo baada ya kundi la Kelele Takatifu kuvunjika.

Katika mahojiano yake hivi karibuni moji amesema maamuzi ya kuvunja kundi hilo yalikuwa magumu kiasi cha kumuathiri kisaikolojia.

Msanii huyo amesema aliogopa kufeli kimuziki walipoanzisha shughuli zao za usanii kama wanamuziki wa kujtegemea na mwanachama mwenzake Didi Man ikizingatiwa kuwa makundi yaliyovunjika kipindi cha nyuma wasanii wake walipotea kimuziki.

Moji ambaye anafanya vizuri na ngoma yake iitwayo Kameshika kwa sasa yupo kwenye media tour yake Cheza Gospel inayolenga kubadilisha tasnia ya muziki wa injili nchini ambayo amedai imekuwa ikisuasua katika siku za hivi karibuni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke