You are currently viewing MONI CENTROZONE ATHIBITISHA KOLABO YAKE  NA MSANII WA KONDE GANG, ANJELLA

MONI CENTROZONE ATHIBITISHA KOLABO YAKE NA MSANII WA KONDE GANG, ANJELLA

Female singer kutoka lebo ya Konde Gang Worldwide, msanii Anjella huenda tukamsikia kwenye ngoma ijayo ya rapa Moni Centrozone.

Rapa huyo mzaliwa wa Majengo Sokoni, Dodoma kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share picha akiwa na Anjella na kueleza kwamba angetamani mrembo huyo asikike kwenye moja ya ngoma yake, ikiwa ni kolabo yake ya kwanza na msanii wa kike.

“Queen anjella Watu wa Majengo itabidi utuchapie kibwagizo kwenye mdundo mmoja wa HipHop. Itakuwa collabo yangu ya kwanza na msanii wa kike”. Aliandika Moni kwenye Instagram page yake.

Sanjari na hilo, wawili hao Jumamosi hii iliyopita walishusha burudani kwenye jukwaa la tamasha la Harmonize, Afro East Carnival, jijini Dar es salaam.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke