Timu ya taifa ya Morocco imefanikiwa kuvuna jumla ya dola za Kimarekani milioni 25 sawa na Ksh. bilioni 3 baada ya kufanikiwa kumaliza nafasi ya nne kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Croatia walioshinda nafasi ya tatu wamejishindia dola milioni 27 sawa na Ksh. bilioni 3.3, mshindi wa pili kati ya Ufaransa na Argentina leo atavuna dola milioni 30 sawa na Ksh. bilioni 3.7 huku bingwa wa michuano akivuna dola milioni 42 sawa na Ksh. bilioni 5.2