Rappa Motra The Future ameachia Extended Playlist (EP) yake mpya inayokwenda kwa jina la “Baba Ako” yenye jumla ya ngoma sita.
Kwenye EP hiyo, Motra awameshirikisha wasanii kama G Nako, Jaivah na Bytar Beast.
Ngoma zinazopatikana kwenye Ep yake ni pamoja na “On Fire”, “Wauwe”, “Pisi Mawenge”, “How we do”, “A Town” na “Wape”.
Motra The Future ambaye ni rapa kutoka Tanzania, EP hii inaenda kuwa project yake ya tatu kuiachia mwaka huu. Ameshaachia ngoma kama “Chips” na “Amor” pia ana documentary yake (mpya) kupitia channel yake ya youtube ambapo amezungumzia safari yake nzima ya muziki