You are currently viewing Mr. Seed afunguka chanzo cha kumaliza ugomvi wake na Bahati

Mr. Seed afunguka chanzo cha kumaliza ugomvi wake na Bahati

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Seed amefichua kuwa waliamua kumaliza ugomvi wao na Bahati kwa manufaa ya watoto wao.

Kwenye mahojiano na World IS, Mr. Seed amesema watoto wao walikuwa wakishambuliwa kila mara kwenye mitandao ya kijamii kutokana na utofauti wao kimuziki, kitendo kilichowalazimu kukutana na kuweka kando uhasama wao ambao ungeathiri ukuaji wa watoto wao katika siku za mbeleni.

“Nilikuwa nikiposti picha za mtoto wangu Gold na mashabiki wenye roho chafu walikuwa na mazoea ya kumlinganisha na mtoto wa Bahati Majesty. Hilo pia lilitokea kwa upande wa Bahati na watoto wetu wangeishia kutusiwa,” Alisema.

Mr. Seed na Bahati ambao walikuwa marafiki wa karibu, walitofautiana mwaka 2018 baada ya wake zao Diana Marua na Nimo Gachuiri kukosa maelewano katika hafla ya mkesha wa mwaka mpya.

Kwa mujibu wa mashuhuda, Diana alipinga wazo la Nimo la kuuza kahawa na vitafunio kwenye sherehe hiyo na aliishia kuwapigia simu polisi kumuondoa Nimo ambaye kwa wakati huo alikuwa mjamzito mzito.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke