You are currently viewing MR. SEED AFUNGUKA MAZITO KUHUSU UKARIBU WAKE NA BAHATI

MR. SEED AFUNGUKA MAZITO KUHUSU UKARIBU WAKE NA BAHATI

Msanii nyota nchini Mr Seed amemuandika waraka mrefu msanii mwenzake Bahati baada ya hitmaker huyo wa ngoma ya Adhiambo kuweka wazi azma yake ya kuwania ubunge wa Mathare kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Kupitia waraka huo ambao aliuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram Mr. Seed ameeleza namna alivyokula maisha ya taabu na bahati wakiwa wanaishi mathare, kipindi ambacho walikuwa wanajaribu kupenya kwenye kiwanda cha muziki nchini.

Kulingana na Hitmaker huyo wa ngoma ya “Around”, umaskini ulikuwa sehemu ya maisha yao na haikuwazuia kuwaza mambo makubwa ambayo walikuwa wanatamani kufanikisha katika maisha yao.

Mr. Seed ambaye ni bosi wa lebo y muziki ya Starbon ametangza kumuunga mkono bahati kwenye azma yake ya kuwa mbunge wa mathare kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka wa 2022 ambapo amemtaja msanii huyo kama kiongozi ambaye anawafaa wakaazi wa eneo hilo.

Itakumbukwa mapema mwaka wa 2019 mr seed waliingia kwenye bifu na bahati baada msanii huyo kuigura lebo ya muziki ya EMB ambako alikuwa amesainiwa kwa kipindi cha miaka miwili. Lakini ilikuja ikabainika baadae kuwa bifu ya wawili hao ilisababishwa na ugomvi ulioibuka kati ya wake zao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke