Staa wa muziki nchini Mr. Seed ameonekana kutofurahishwa na miendo ya mfanyibiashara aliyeugikia siasa Jimmy Wanjigi.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Mr. Seed ameandika ujumbe wa masikitiko kwenda kwa wanjigi akisema kwamba mwanasiasa huyo ameshindwa kumlipa pesa zake licha ya kutoa huduma kwenye hafla yake ya siasa majumaa kadhaa yaliyopita.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Dawa ya Baridi” amesema Wanjigi amekuwa jeuri kwenye suala la kumlipa deni lake kwani kila mara akimuulizia kuhusu deni lenyewe amekuwa akitoa ahadi za uongo ambazo mpaka hajaweza kutimiza.
Hata hivyo suala hilo limeibua maswali mengi miongoni mwa Wakenya kwenye mitandao ya kijamii ambapo wameonekana kumlaumu Mr. Seed kwa kukubali kufanya kazi na mwanasiasa bila ya kuwa na mkataba wa maelewano.
Utakumbukwa hii sio mara ya kwanza kwa Jimmy Wajingi kukosa kuwalipa watoa huduma kwenye shughuli zake kwani kipindi cha nyuma alituhumiwa pia kukwepa kulipa madeni ya wanamitindo wa mavazi waliyompa huduma.