You are currently viewing MR. SEED AMPA MKE WAKE GARI AINA MAZDA DEMIO KAMA ZAWADI YA KRISMASI

MR. SEED AMPA MKE WAKE GARI AINA MAZDA DEMIO KAMA ZAWADI YA KRISMASI

Wakati ukichukulia poa mahusiano yako na mpenzi wako, Staa wa muziki nchini Mr. Seed hakuwa na jambo dogo kwa Baby Mama wake Nimo , kwani amempatia zawadi ya gari aina Mazda Demio yenye thamani ya shillingi millioni 1.2.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mr Seed amesema amenunua gari hilo akiwa na imani siku moja atakuwa na uwezo wa kumzawadi mke wake gari aina ya Range Rover.

Nimo ametoa shukrani za dhati kwa mumewe kwa zawadi hiyo ya kitofauti ambayo hakuitegemea, sambamba na kuonyesha gari hilo pamoja na bei kupitia risiti ya manunuzi.

Mr. Seed ambaye anamilika gari aina Toyota Mark X kwenye mahojiano mbali mbali amenukuliwa akimsifia  mke wake Nimo kwamba amempambania kwenye shida na raha.

Hitmaker huyo “Dawa ya Baridi” amesema kuna kipindi alitaka kuchukua maamuzi magumu ya kuacha muziki lakini baby mama wake Nimo alikuwa mstari kumtia moyo asikate tamaa kwenye harakati za kuupeleka muziki wake kwenye level nyingine.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke