Nyota wa muziki nchini Mr. Seed ameibuka na kumtaka staa wa muziki wa nyimbo za injili Ringtone kuoa.
Msanii huyo amedai kwamba Ringtone ameshakuwa mtu Mzima, hivyo anaamini kuwa akioa itamletea heshima sana katika jamii.
Akiwa kwenye moja ya interview Mr. Seed amesema majukumu ya ndoa pekee ndiyo yatamnyamazisha Ringtone ambaye katika siku za hivi karibu amekuwa gumzo mitandaoni kutokana na sarakasi zake.
Hitmaker huyo wa “Dawa ya Baridi” amesema amechoshwa na mienendo ya Ringtone kuingilia ndoa za wasanii wenzake kila mara ikizingatiwa kuwa yeye binafsi ameshindwa kumpata mwanamke wa ndoto yake.
Hata hivyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba ringtone ni msherati namba moja ambaye amejificha kwenye muziki wa injili kwani amekuwa na mazoea ya kuzama kwenye DM za warembo wa Instagram akiomba penzi.
Kauli ya mr seed imekuja mara baada ya ringtone kuonekana kumshambulia kila mara kwenye interviews mbali mbali kufuatia hatua yake ya kuanza kuimba nyimbo za mapenzi tofauti na muziki wa injili ambao ulimtambulisha kwenye kiwanda cha muziki nchini