Msanii nyota nchini Mr. Seed anazidi kujipakulia baraka ya wazazi wake mara baada ya kumzawadi mama yake mzazi kipande cha ardhi ambacho ana mpango wa kumjengea mjengo wa kifahari.
Kupitia video aliyoiposti kwenye ukurasa wake wa Instagram Bosi huyo wa lebo ya muziki ya Starborn Empire ametusanua kuwa shamba hilo aliyomnunulia mama yake lipo eneo la Matuu, Kaunti ya Machakos.
Hakuishia hapo ameenda mbali zaidi na kutoa ushuhuda wa ndani ya maisha yake kwa kusema kwamba kuna kipindi familia yake ilipitia maisha magumu kiasi cha kukosa chakula kila siku.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Ndoa” amewahimiza vijana na mastaa wenzake kukumbuka wazazi wao wanapofanikiwa kimaisha kwa kuwanunulia vitu vya thamani kwani bila wao wasingeweza kufanikisha baadhi ya malengo yao.
Utakumbuka mwaka wa 2018 Mr. Seed alimzawadi mama yake mzazi gari mpya aina Toyota Audi kwa kuwa mama bora kwake lakini pia mwaka wa 2021 aliingia kwenye headlines nchini alipomnunulia mke wake Nimo gari mpya aina ya Mazda Demio kwa kusimama nae kipindi ambacho alikuwa amefulia kiuchumi.