Nyota wa muziki nchini Mr. Seed ameweka wazi kuachia remix ya smash hit yake iitwayo “Dawa ya Baridi”. Wimbo ambao bado unaendelea kufanya vizuri kupitia majukwaa mbalimbali ya ku-stream muziki mtandaoni.
Mr Seed ametangaza uwepo wa remix hiyo kupitia mahojiano yake na nicholas kioko ambapo amedokeza mpango wa kumshirikisha mbosso kutoka WCB kwenye remix ya wimbo wa dawa ya Baridi.
Katika hatua nyingine amethibitisha pia kujikita zaidi katika suala la kufanya kolabo na wasanii mbali mbali ndani ya mwaka huu tofauti na mwaka jana alipokuwa anajishugulisha na kazi zake za muziki kama msanii wa kujitegemea.
Utakumbuka kwa sasa Mr. Seed anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Pressure aliyomshirikisha Nviiri the story teller ambao una zaidi ya views laki 2 youtube ndani ya wiki moja.