You are currently viewing MRATIBU WA BRIGHT FUTURE CONCERT BIANCA AMVUA NGUO MASAUTI, AWEKA HADHARANI MADHAIFU YAKE.

MRATIBU WA BRIGHT FUTURE CONCERT BIANCA AMVUA NGUO MASAUTI, AWEKA HADHARANI MADHAIFU YAKE.

Mratibu wa tamasha la Bright Future lililofanyika majuzi mjini Mombasa Bianca amekanusha taarifa za kutomlipa staa wa muziki nchini Masauti

Akipiga stori na Mvumo Extra kwenye mtandao wa Youtube Bianca amesema kwamba msanii huyo alilipwa pesa zake ambapo amefichua kuwa ana riziti zote zinazonyesha Masauti alilipwa haki yake.

Bianca, ambaye ni mtaalam wa Mahusiano ya Umma amesikitishwa na hatua ya Masauti kusema hakupewa huduma za usafiri kwenye tamasha la Bright Future kwa kusema kwamba walifanya kila liwezalo kumweka msanii huyo sawa ila Masauti na uongozi wake kwa kwenda kinyume na mkataba wa maelewano.

Bianca amesema amejaribu kuwasiliana na Masauti ili kutatua tofauti ambazo zilitokea baada ya shoo kumalizika lakini msanii huyo ameingiwa na jeuri kwani hachukui simu zao. Amemtaka Masauti ache kiburi na badala yake washirikiane nao ili wazike tofauti zao ambazo zilitokea wakati wa tamasha la Bright Future

“Masauti, watu kadhaa wamewasiliana nawe lakini umekataa kuchukua simu. Tafadhali fanya kinachohitajika, acha aibu,” alisema Bianca katika mahojiano na Mvumo Extra kwenye mtandao wa YouTube.

Kauli ya Bianca imekuja mara baada ya taaarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kwamba Masauti na Nadia Mukami waliamriwa kuondoka jukwaani kwa lazima ili kutoa nafasi kwa msanii wa bongofleva Mbosso atumbuize.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke