You are currently viewing MREMBO AMINA MUADDI AKANUSHA KUVUNJA PENZI LA RIHANNA NA ASAP ROCKY

MREMBO AMINA MUADDI AKANUSHA KUVUNJA PENZI LA RIHANNA NA ASAP ROCKY

Mrembo mbunifu wa viatu Amina Muaddi ameibuka na kukanusha taarifa za kulivunja penzi la Rihanna na Asap Rocky.

Kupitia insta stories kwenye mtandao wa Instagram, mrembo huyo ameandika kwamba ameamua kufunguka kwa sababu taarifa hizo zinamvunjia heshima kwa kuwa Rihanna & A$AP Rocky ni watu ambao ana waheshimu kwa kiasi kikubwa sana.

Kauli ya Mrembo huyo inakuja mara baada ya Mtu wa karibu na wawili hao kuuthibitishia mtandao wa TMZ kuwa stori za A$AP Rocky kumsaliti Rihanna na zile za kuachana hazina ukweli kwani wapenzi hao wako vizuri.

Mapema jana ziliibuka stori hizo kupitia twitter na kusambaa kwenye mitandao yote duniani kwamba Riri ambaye ni mjamzito, ameachana na rapa AsapRocky mara baada ya kugundua kuwa anamsaliti kwa kutoka kimapenzi na mrembo mbunifu wa viatu kwenye kampuni ya Riri, Fenty aitwaye Amina Muaddi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke