You are currently viewing MRISHO MPOTO ASHANGAA WASANII WAKUBWA WA BONGOFLEVA KUIMBA AMAPIANO

MRISHO MPOTO ASHANGAA WASANII WAKUBWA WA BONGOFLEVA KUIMBA AMAPIANO

Msanii mwenye mashairi yaliyoshiba kutoka nchini Tanzania Mrisho Mpoto ameeleza kushangaa na namna wasanii wa Bongofleva wanavyokilimbilia kufanya muziki wa Amapiano kutoka Afrika Kusini.

Kwenye mahojiano na E FM Mpoto amesema kuna wasanii wakubwa nchini Tanzania wana kila kitu katika muziki wao lakini anashangaa ni kipi hasa wanakitafuta kwenye Amapiano.

“Unakuta mpaka malegendary wakubwa wameingia kwenye Amapiano wote, ukisikikiza mpaka unajiuliza hata huyu, anatafuta nini sasa kiki au anatafuta hela wakati anayo, huyu ndio angekuwa kioo, angekuwa njia”.

“Kuna na Amapiano zimetoka juzi nimeshtuka sana niliogopa nusu niipaki gari niingie chini ya uvungu” amesema Mrisho Mpoto katika Joto la Asubuhi, E FM Radio.

Inaelezwa kuwa muziki wa Amapiano ulianza mwaka 2012 huko nchini Afrika Kusini,ingawa wapo wanaodai ulianzia katika vitongoji vya Johannesburg na Soweto kisha ikasambaa kote Afrika na baadhi ya maeneo duniani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke