You are currently viewing MRITHI WA OLE GUNNAR KITENDAWILI ULAYA

MRITHI WA OLE GUNNAR KITENDAWILI ULAYA

Kocha wa Paris St-Germain ambaye ni raia wa Argentina Mauricio Pochettino anatajwa kuwa kwenye kipaumbele cha kwanza katika kazi ya kuinoa Manchester United baada ya klabu hiyo kumfuta kazi ya ukocha Ole Gunnar Solskjaer, makocha wengine ni kocha wa Ajax Erik ten Hag na Zinedine Zidane.

Manchester United imefanya mazungumzo tena na kocha wa Leicester City Brendan Rodgers, ambapo kumpata kwake lazima ulipe fidia kiasi cha pauni milioni 8. Imeelezwa.

Wakala wa Kireno Jorge Mendes anaendelea kupambana kuhakikisha kocha wa Sevilla na kocha wa zamani wa Real Madrid Julen Lopetegui anachukua urithi wa Ole Gunnar Solskjaer Manchester United. Mkataba wa mhispania huyo unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2024.

Hata hivyo, kocha wa Hispania Luis Enrique amekanusha vikali taarifa za kuhusishwa kujiunga na Manchester United

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke