Msanii chipukizi nchini Kenya, Kush Paula amejipata pabaya mtandaoni mara baada ya kutuhumiwa kuhusika kwenye wizi wa mdundo wa wimbo uitwao “Mdaka Mdakiwa” wake Sanaipei Tande.
Walimwengu kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram wanadai kwamba mrembo huyo alisample mdundo wa wimbo huo na kisha akautumia kwenye wimbo wake uitwao Dodo ambao kwa asilimia 100 unafanana kabisa na wa Sanaipei Tande.
Hata hivyo watu wengi wameonekana kumyoshea kidole cha lawama prodyuza aliyetayarisha wimbo wa Kush Paula wakidai kuwa amekosa ubunifu wa kutengeneza beat nzuri ambayo ingemfaa mrembo huyo huku wengine wakimtaka Sanaipei Tande achukue hatua ya kuushusha wimbo wa “Dodo” kwenye mtandao wa Youtube kwa madai ya Hakimiliki.
Ikumbukwe wimbo wa “Dodo” wake Paula ulitoka mwezi Oktoba mwaka 2021 na mpaka sasa inazaidi ya views 1,344 Youtube huku “Mdaka Mdakiwa” wake Sanaipei Tande ukiachiwa rasmi mwezi Mei mwaka 2020 na ina zaidi ya views millioni 2 kwenye mtandao wa Youtube.