You are currently viewing Msanii Fat S afunguka kuhusu ugomvi wa Dazlah na T-Hits

Msanii Fat S afunguka kuhusu ugomvi wa Dazlah na T-Hits

Msanii Fat S amewapa somo prodyuza T-Hits na aliyekuwa msanii wake Dazlah mara baada ya wawili hao kuingia kwenye ugomvi.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Fat S amesema hatua ya wawili hao kuwekeana vikwazo kwenye shughuli zao za muziki imeleta taswira mbaya kwenye jamii lakini pia imerudisha nyuma juhudi za kukuza muziki wa Pwani.

Hata hivyo amemtaka Prodyuza T-Hits na Dazlah kuweka kando tofauti zao na badala yake washirikiane kwa manufaa ya tasnia ya muziki.

Kauli ya Fat S imekuja mara baada ya kudaiwa kuwa Prodyuza T-Hits hakufurahishwa na hatua ya Dazlah kujiunga na uongozi wa Shirko Media ikizingatiwa kuwa yeye ni moja kati ya watu ambao walimtoa kimuziki msanii huyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke