You are currently viewing MSANII MPYA WA TNS RAHMAH PINKY AAPA KUVUNJA REKODI YA SHEEBAH KARUNGI

MSANII MPYA WA TNS RAHMAH PINKY AAPA KUVUNJA REKODI YA SHEEBAH KARUNGI

Baada ya kuachia singo yake ya kwanza iitwayo “Superstar”, msanii mpya aliyechukua nafasi ya Sheebah Karungi kwenye lebo ya muziki ya Team No Sleep, Rahmah Pinky ameibuka na kujinasibu kuwa anaenda kuvunja rekodi ya Sheebah kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda kwa kuachia hits kali bila kupoa.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 17 amesema atafanikisha hilo kupitia kipaji chake cha uandishi wa nyimbo na ukubwa wa uongozi wake.

“Sina ushindani na Sheebah, lakini nataka kufanikiwa zaidi kimuziki kuliko yeye. Nitatumia ujuzi wangu wa kuandika nyimbo kufanikisha hilo,” alisema katika mahojiano na runinga moja  nchini Uganda.

Kadhalika, amesema atafanya kazi kwa bidii kama njia ya kumjengea msingi wa mashabiki ambao watamsaidia kupenya kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.

Hata hivyo Rahmah Pinky amesema kuwa anamheshimu sana Sheebah kama mtu ambaye alifungua milango kwa wasanii wengi wa kike nchini Uganda.

Utakumbuka mwishoni mwa mwaka wa 2021 Sheebah Karungi aliigura lebo ya muziki ya Team No Sleep hii ni baada ya kuingia kwenye ugomvi wa mali na meneja wa Jeff Kiwa.

Baada ya Sheebah kuondoka Jeff Kiwa alienda mbali zaidi na kumtambulisha Rahmah Pinky kama msanii mpya wa TNS kujaza pengo liloachwa na Hitmaker huyo wa Boy fire.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke