Msanii mpya wa Team No Sleep Rahamah Pinky amekanusha tuhuma za kumuibia msanii chipukizi nchini Uganda Morgan Gloria wimbo wake wa Superstar.
Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni Pinky amesema meneja wake jeff kiwa alinunua wimbo huo kutoka kwa mwandishi mmoja wa nyimbo ambaye hakuweka wazi jina lake.
Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 17 amemtaka Morgan Gloria kumtafuta mwandishi huyo wa wimbo wake Superstar watatue tofauti zao badala ya kuichafulia jina lebo yake ya Team No Sleep kwa tuhuma za uongo.
Kauli ya Pinky imekuja mara baada ya Morgan Gloria kunukuliwa kwenye moja ya interview akidai kwamba atamfungulia mashtaka msanii huyo wa TNS kwa madai ya kumuibia wimbo wake wa superstar ambao tayari alikuwa amerekodi na lebo hiyo.