Mwanamuziki wa Kenya Sheila Wairimu maarufu kama Shay Diva amepatikana na hatia ya kuiba gari aina ya Land cruiser V8 kutoka mpenzi wake.
Hakimu mkaazi wa mahakama ya Kitale Julius N’garng’ar amesema Shay Diva alihamisha umiliki wa gari hilo katika mazingira ya kutatanisha siku moja tu baada ya kifo cha mpenzi wake .
Shay Diva anatarajiwa kuhukumiwa tarehe 5 Desemba 2022 kufuatia kukiri umiliki wa gari hilo ulibadilisha bila ya yeye kushirikishwa.
Ikumbukwe Mwanamuziki huyo alishtakiwa kwa kuingia kwenye akaunti ya TIMs/NTSA ya bwenyenye PJ Dodhia Kumar na kuhamisha umiliki wa gari hilo kwake bila kufuata taratibu stahiki za umiliki.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 61 alifariki dunia Aprili 2021 na baada ya familia yake kubaini kuwa Shay Diva alikuwa amechukua gari hilo kwa njia ya utata, waliahamua kufungulia mashtaka.