You are currently viewing MSANII WA BONDOCKS GANG EXRAY TANIUA ATHIBITISHA UJIO WA KOLABO ZAKE MBILI NA WASANII WA NIGERIA

MSANII WA BONDOCKS GANG EXRAY TANIUA ATHIBITISHA UJIO WA KOLABO ZAKE MBILI NA WASANII WA NIGERIA

Msanii nyota nchini Exray Taniua anazidi kuchana mbuga kimataifa hii ni baada ya kutangaza ujio wa kolabo zake na wasanii nyota nchini Nigeria.

Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Exray amethibitisha kuwa ana kolabo mbili na simi pamoja Mr. Eazi ambapo amewataka  mashabiki zake wampe ushauri ni kolabo gani kati ya wasanii hao aachie kwanza.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wamependekeza aachie kolabo zote mbili huku wengine wakimshauri aachia kola yake na Simi kwani moja kati ya wadada ambao muziki wao unawakosha.

Huu ni muundelezo mzuri kwa Exray ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akiachia nyimbo bila kupoa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke