You are currently viewing MSANII WA BONGOFLEVA KILLY AACHIA RASMI EXTENDED PLAYLIST (EP) YAKE MPYA

MSANII WA BONGOFLEVA KILLY AACHIA RASMI EXTENDED PLAYLIST (EP) YAKE MPYA

Mwanamuziki kutoka Konde Gang Worldwide Killy ameachia EP yake mpya inayokwenda kwa jina la The Green Light.

Killy ameamua kuwa surprise mashabiki zake kwa kuachia EP hiyo mpya yenye nyimbo5 za moto huku ikiwa na kolabo mbili tu kutoka kwa Christian Bella, Harmonize na Ibraah.

The Green Light EP ina nyimbo kama Ni Wewe, Vumilia, Kiuno, Itafika, Ilete, Niambie na itapatikana kwenye  Digital Platforms za kusambaza muziki duniani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Killy amewashkuru maprodyuza na wasanii wenzake kwa kushirikiana nae kwenye mchakato wa kuiandaa ep hiyo.

Hii inakuwa EP ya kwanza kutoka kwa mtu mzima Killy tangu atambulishwe kama msanii wa lebo ya muziki ya Konde Gang Worldwide inayomilikiwa na Harmonize.

 

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke