Msanii mkongwe wa Bongofleva, Q Chief amesema haimuingi akilini kabisa suala la Saraphina kufananishwa na Vanessa Mdee kwenye muziki.
Katika mahojiano yake na EATV, Q Chief amesema Saraphina anafanya vizuri kimuziki lakini nafasi ya Vanessa ipewe heshima yake.
“Viatu vya mtu visivaliwe na mtu mwingine, yaani mnataka kumfananisha Saraphina na Vanessa Mdee kweli? anafanya vizuri kwenye game lakini tuheshimu kile tunachokiona kila siku” Q Chief ameimbia EATV.
Saraphina ambaye ni mshindi wa Bongo Star Search (BSS) 2021 wikiendi iliyopita alishinda tuzo mbili za Tanzania Music Awards (TMA).
Utakumbuka Vanessa Mdee alishatangaza kuachana na muziki wa Bongofleva, kabla hapo aliweza kushinda tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA), All Africa Music Awards (AFRIMA) na nyinginezo.